Rigathi Gachagua Aapa Kutoa Ushahidi Kuhusu Utawala wa Rais Ruto
Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amejitokeza wazi kuwa yuko tayari kutoa ushahidi kuhusu utawala wa Rais William Ruto, ikiwa ni pamoja na madai ya uhusiano wa kifedha na kisiasa na mataifa kama China, Urusi, na Iran.
Gachagua amesema hana hofu ya kuhojiwa kuhusu matamshi aliyoyatoa akiwa Marekani, ambapo alielezea hali ya kisiasa nchini Kenya akisema:
"Shida si Kenya, shida ni Ruto."
Aidha, Gachagua amekataa wito wa Waziri wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, kumtaka aandikishe taarifa kuhusu matamshi yake, akisisitiza kuwa hana cha kuomba msamaha.
Gachagua amesisitiza kuwa yuko tayari kushirikiana na uchunguzi wowote wa kisheria kutoka kwa vyombo vyote vinavyohusika, ili kufichua ukweli kuhusu uhusiano wa utawala wa Rais Ruto na masuala ya usalama wa ndani na nje ya nchi.
Aliiondolewa mamlakani mwezi Oktoba 2024 baada ya kutofautiana na Rais Ruto, na tangu wakati huo amekuwa akielezea hadharani mtazamo wake kuhusu utawala wa sasa. Kwa sasa, Gachagua anatumia mitandao ya kijamii na redio za lugha za mama kufikisha ujumbe wake kwa wafuasi, baada ya mikutano yake ya hadhara kuzimwa mara kadhaa.
Kwa maelezo zaidi, soma makala kamili kwenye Taifa Leo.
Comments
Post a Comment